WATU 57 wameuawa na wengine 60 kujeruhiwa katika shambulizi la kujitoa muhanga karibia na eneo lenye misikiti miwili wakati wa muendelezo ya sherehe za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad, nchini Pakistan, qReuters wameripoti.
–
Imeelezwa hakuna kundi lililodai kuhusika na milipuko hiyo.
–
Vyombo vya habari mbalimbali duniani vinaripoti kuwa kuongezeka kwa mashambulizi ya wanamgambo kumeongeza hatari kwa vikosi vya usalama kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Januari.
–
Mlipuko wa kwanza, katika Mkoa wa Kusini magharibi wa Balochistan, uliua watu 52, kulingana na afisa wa afya wa wilaya, Abdul Rasheed.
–
“Mshambuliaji alijilipua karibu na gari la polisi karibu na Msikiti wa Madina ambapo watu walikuwa wakikusanyika kwa maandamano,” aliongeza afisa mkuu wa polisi Munir Ahmed.
–
Shambulio la pili katika eneo jirani la Khyber Pakhtunkhwa kaskazini-magharibi liliua watu watano kwenye msikiti mmoja, kwa mujibu wa maafisa wa uokoaji. Paa la msikiti liliporomoka, mtangazaji wa Geo News alisema, na kuwakandamiza takriban watu 30 hadi 40 chini ya vifusi.
–
Shambulio hilo lilihusisha milipuko miwili, mmoja ukiwa kwenye lango la msikiti na mwingine katika boma hilo, afisa mmoja alisema.
Mlipuko wauwa watu 57 Pakistan
Sign Up For Daily Newsletter
Be keep up! Get the latest breaking news delivered straight to your inbox.
By signing up, you agree to our Terms of Use and acknowledge the data practices in our Privacy Policy. You may unsubscribe at any time.
Rayyan Mvungi
Leave a comment
Leave a comment