⚠️😳 “Nilianza kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza nikiwa na miaka 15 na nilifanya na Madebe Lidai baada ya kunitongoza ili niweze kucheza nae movie, ilikuwa mwaka 2009 lakini hata hivyo hatukufanikiwa kutoka kisanaa tulipotezana hadi tulipokuja kukutana tena miaka kadhaa baadae. Tulipokutana tuliendeleza mahusiano yetu nikafanya nae filamu kadhaa na alinipa kipaumbele kwasababu nilikuwa mtu wake”
“Mimi na Madebe tulifunga ndoa mwaka 2019, mwanzoni ndoa ilikuwa tamu lakini baadae mambo yalianza kubadilika, akawa hanipi kazi tena kwenye kuigiza, akaingiza wivu hata kambini mazoezini nikawa siendi, watu wakinifata kufanya kazi na mimi anawadanganya anawaambia mke wangu hawezi kufanya kazi chini ya milioni tano, anawaambia hivyo kwasababu anajua watashindwa kufika dau kwahiyo nikawa sipati kazi zake wala za wasanii wengine baadae nikajikuta tu nimekuwa mama wa nyumbani”
“Ana wanawake wengi huko kazini ndio maana amenipiga marufuku kwenda mazoezini, huko kuna chumba maalumu cha kupumnzika yeye na mwanamke wake maana hata mimi wakati nipo nae alitenga chumba chetu maalumu, hana utu, ni tofauti na watu wanavyomchukulia huko nje. hana huruma, hadi sasa ameoa wanawake watano na hao wengine wote ameachana nao na nasikia hivi juzi kaniolea mke mwingine”
“Madebe ni mume wangu lakini ananitesa, nimeishi kwenye mateso kwa muda mrefu, nakosa pesa ya kula, sikumbuki ni lini aliacha pesa ya matumizi na huku anajua kabisa nina watoto wake, ananipiga, amenipa talaka mara kadhaa lakini baadae ananiomba msamaha anavunja talaka. Mimi nimechoka lakini naogopa kuondoka nitaaibika. Kuna nyumba yetu ipo Chanika tumejenga wote lakini baada ya nyumba kukamilika akataka amuweke huyo mwanamke wake mpya aliyemuoa”
“Mimi naiomba Serikali kama inanisikia, nipate haki yangu, aniachie nyumba tu yeye aendelee na wanawake zake maana sio mmoja wapo wengi, nimechoka siwezi kwenda kushtaki popote kwasababu watu wanaona kama mimi ndio mgomvi, wanasema hawezi kuwa hivyo kwasababu anawafunda watu kwenye filamu na hata yeye anajisifia kuwa siwezi kumshtaki popote kwasababu anajulikana na watu wanamuamini”- Chanuo