Bei mpya za mafuta ya Petroli na Dizeli zilizotangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na kuanza kutumika chini kote zimeibua manung’uniko kutoka kwa watumiaji huku wakieleza kuwa hali hiyo itasababisha kuongezeka kwa ugumu wa maisha.
Ongezeko hilo la shilingi zaidi ya 400 kwenye kila lita ya petroli na nyongeza ya shilingi zaidi ya 350 kwa kila lita ya dizeli limegusa wengi na hivyo moja ya ushauri uliotolewa kwa serikali ni kuanza kutumia nishati mbadala. Je, ni kwa namna gani nishati mbadala itakuwa mwarobani wa madhara ya kupanda kwa bei hizo?